Mfanyakazi mmoja wa hoteli nchini Uingereza
alilazimika kutoa painti mbili za damu (Takriban
lita moja) kutoka kwenye uume wake- baada ya
kusimama kwa muda wa saa 17 mfululizo.
Madaktari kwanza walijaribu kupunguza kasi ya
damu kwa kijana huyo, Jason Garnett, kwa kupiga
sindano 24 moja kwa moka kwenye nyeti zake.
Tovuti ya Metro imesema 'mashine' ilisimama
kuanzia siku ya Ijumaa asubuhi alipoamka. Kijana
huyo, 23, alijaribu kila aina ya njia, ikiwemo
kukimbia, na kuoga maji ya baridi sana, kabla ya
kupelekwa hospitali na rafiki yake.
Hospitali iligundua kuwa Garnett alikuwa na
maradhi ambayo ni haba kuonekana yajulikanayo
kama priapism - ambapo uume husimama bila
kukoma. Maradhi hayo hayasababishwi na hamu
ya kutaka kufanya mapenzi, lakini iwapo mtu
hatopata tiba, inaweza kuharibu uume, imeripoti
tovuti ya News.com.au.
Akizungumza na gazeti la The Sun, amesema:
"Yaani kuishia hospitali na jambo hili, ni moja ya
siku ya aibu zaidi kwangu duniani.
"Kuona wakichoma sindano 'mashine' yangu
ilikuwa jambo gumu sana kwangu- kama
kutazama filamu ya kutisha. Maumivu yalikuwa
asilimia 100."
Amesema baada ya sakata hilo, nyeti yake ina
majeraha 'kibao'.
Search This Blog
Tuesday, 7 October 2014
APELEKWA HOSPITALI BAADA 'MASHINE' KUSIMAMA KWA SAA 17
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
what you think?