Search This Blog

Saturday, 6 September 2014

WATAALAMU WA AFYA WASHAURI KULALA BILA NGUO ZA NDANI WAKATI WA USIKU

Madaktari na waalamu wa afya wanashauri
kulala bila nguo za ndani wakati wa usiku ili
kuwezesha viungo vya uzazi kupata hewa ya
kutosha ili kuepuka maambukizi ya fangasi na
kutoa harufu mbaya katika sehemu za siri.
  Kuvaa nguo za ndani wakati wa kulala
husababisha kubana sehemu za siri na joto
kupita kiasi ambayo usababisha unyevu na
kuvutia ukuaji wa fangasi na bakteria kwa jinsia
zote huku pia zikisababisha upungufu wa
mbegu za kiume na harufu mbaya.
Tambua kuwa joto la mwili hushuka kiasi
unapolala na kukuwezesha kupata usingizi
mzuri wakati wa usiku hivyo kulala na nguo za
ndani au nguo zozote zinazobana ni kinyume
chake na huongeza mikunjo kwenye ngozi na
kupunguza uzuri wa ngozi.
Ikumbukwe kuwa hii haiwahusishi wanawake au
wanaume wenye matatizo maalumu
yanayowapasa kuvaa nguo za ndani usiku
kama hedhi kwa wanawake na matatizo ya
uzazi.
Hivyo ni muhimu kulala bila nguo za ndani au
nguo zinazobana mwili wako ili kuepuka
madhara haya.

Source: WHO kupitia jamiiforums

No comments:

Post a Comment

what you think?